Header Ads

Header ADS

Nyumba yaungua moto kwa shoti ya umeme

          Nyumba moja iliyopo  mtaa wa Mangula  katika Halmashauiri ya Mji Mdogo wa Makambako Mkoani Njombe  ambaye inamilikiwa na familia ya Chaula.Imeungua moto ikiwa chanzo ni hitilafu ya umeme.

     Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mangula  bwana Shabani Selemani  Ngilimbe ,ambaye kimjibu amebainisha kuwa hakuna madhara yaliyotokana na moto huo kwa kuwa wananchi walikuwa wamesha wahi kuuzima moto.
        Kwa mjibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanabainisha kuwa baada ya kuona moshi unatoka na huku mwenye nyumba akiwa hayupo kwenye eneo la tukio ndipo ikawalazimu kwenda kuibomoa milango kwa nguvu ili waweze kunusuru mali na vitu mbalimbali vilivyo kuwemo ndani ya nyumba.
         Ingawa Jeshi la Polisi la zima moto lilifika katika eneo la tukio bado wananchi wamelinoshea vidole kwa kuchelewa kufika mapema katika eneo la tukiona ikiwa taarifa walikuwa wamesha zipata.

 Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Serikali  ya Mtaa wa Mangula hakuna madhara yaliyojitokeza na kwa kuwa wananchi waliwahi katika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada wa kuokoa na hakuna mtu aliyeathirika kutokana na tukio hilo.




















        Kwa mjibu wa wanafamilia kutoka nyumba hiyo wanakili kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa hakuna madhara  makubwa yaliyoji tokea zaidi japo itakuwa imewarudisha nyuma kimaendeleo kwani kuna baadhi ya madhara ambayo yamejitokeza wakati wa uokoaji ,ikiwemo kubomoa milango na madirisha kwa ajili ya kuokoa mali zilizomo ndani ya nyumba.

                           Ina ripotiwa na mwandi  .
                                George Mwita











No comments

Powered by Blogger.