Header Ads

Header ADS

Watu watatu mbaroni kwa wizi wa meno ya tembo

                       Watu watatu wakiwemo askali jamii wamefikishwa katika mahakama ya hakimu kazi kisutu kwa tuhuma ya kesi ya uhujumu uchumi baada ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya sh 239.5 Milioni .Kwa mjibu wa  Wakili wa Serikali Faraja Nguka ,mbele ya Hakimu Mkazi ,All Salum, amesema washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi  namba 45 ya mwaka 2018.
       















    Pia washitakiwa hao amewataja majina yao kuwa ni .Juma Myali [35], Greyson Mhapa[ wakiwa ni polisi jamii] pamoja na Kefas Mlinzi ,Dereva na Mkazi wa Mbezi Luisi ,Washitakiwa hao kwa pamoja walikamatwa  Juni 28 ,2018 katika eneo ya Mbezi Wilaya ya Ubungo wakiwa na vipande 30 vya meno ya Tembo .
              Aidha inasemekana kuwa vipande hivyo vya meno ya Tembo vina jumla ya thamani za dola 105000 za Kimarekani sawa na 23950,5000 Pasipo kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori.Kwa pamoja watuhumiwa baada ya kusomewa shitaka hilo hawakurusiwa kuzungumza kitu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo .
             Pia upande wa mashitaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyobado haujakamilika  na kuahirishwa mpaka Julai 23,2018.

No comments

Powered by Blogger.