Header Ads

Header ADS

Mawaziri wawili Nchini Uingereza wajiuzulu

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza  amejiuzulu leo baada ya Waziri aliyesimamia  uratibu wa masuala ya kujiondoa kwa Nchi hiyo kutoka umoja wa Ulaya Brexit ,kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo Theresa May.














          Kwa njibu wa taarifa iliyotolewa hii leo makao makuu  ya Waziri Mkuu ,10Downing Street  ,imesemakuwa Bi May ,alikuwa amepokea barua ya kujiuzulu kwa Waziri Jonhson  na kumsifu kwa utenda kaziwake.
   Ikumbukwe kuwa mapema hii leo Waziri ,David Davis , wa maswala ya Brexit ,alikuwa amekiambia kituo cha utangazaji cha BBC kwamba Uingereza haidai hakiyake katika mchakato huo wa kujiondoa katika umoja wa  huo wa muungano wa Ulaya.














                  Kutokana na kujiuzulu kwa Mawaziri hao  inaripotiwa kuwa nipigo kubwa kwa Waziri Mkuu Theresa May na mstakabali wake wa kisiasa.Baada ya muda mfupi kujiuzulu kwa Johnson .Waziri Mkuu May, alihutubia Bunge la Nchi hiyo  na kutetea hatua anazo zichukua katika mchakato mzima wa Brexit .

No comments

Powered by Blogger.