Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,imewakemea Maafisa ushirka wenye visingizio.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ameonyo tabia ya kutowajibika miongoni mwa watumishi kwa kisingizio cha mgawanyo wa madaraka .Kauli hiyo imetolewa wakati akizungumaz na wanaushirika wa Jiji la Mwanza pamoja na wakazi waliojitokeza wa Jiji hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.
Aidha Majaliwa ,amesema kuwa kuna baadhi ya Maafisa ,ambao hawataki kuwajibika kwa sababu wameajiliwa na TAMISEMI ,na wengine wapo chini ya Tume ya maendeleo ya ushirika. Afisa ushirika wa Wilaya yuko Mkoani ambako ni chini ya TAMISEMI ,Mrajis msaidizi wa Mkoa uko Wizarani ,Serikali ni moja kwa hiyo wote bado mnawajibika kwa Mrajis Msaidizi wa Mkoa ,, Alisema , Majaliwa.
Majaliwa amewataka Wakurugezi wa Halmashauri ,wasiwapangie kazi nyingine zilizo nje na taaluma zao .Maafisa hao wa Wilaya wa hakikishe wanatoa taarifa kwenye vikao vya Halmashaaauri zao.'' Ameendelea kusema kuwa msimpe kazi ya kufundisha Afisa ushirika kwa sababa hakuna mtu
mwingine Afisa ushirika aachwe afanye kazi ya ushirika na atoe taarifa` kwenye vikao vyenu. Madiwani mnapo kuwa kwenye baraza, mpeni Afisa ushirika aeleze maendeleo ya ushirika yakoje katika wilaya yenu''
Pia majaliwa amesema changamoto nyingine zinazo ikabili sekta ya ushirika ni wizi na ubadhirifu miongoni mwa watendaji wa vyama vya ushirika walio pewa dhamana ya kuvisimamia na kuviendesha vyama hivyo..
Imetumwa na mwandishi wetu
Adamu Linusi Lupumbwe Kutoka Mwanza.
No comments
Post a Comment