Vijana wawili wachimbaji wa Visima katika Mji wa Makambako wamefariki dunia
Wachimbaji wa wili wa Visima vya Maji kwa kutumia mikono katika Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe wamefariki dunia wakati wakiwa wanasafisha kizima cha Maji kinachomilikiwa na Mlando ambaye anamiliki vyoo vya kulipia vilivyopo nyuma ya Stendi mpya Makambako.
Mwenyekiti wa eneo la Stendi ambapo tukio limetokea Bwana Absalm Magoma amewataja marehemu kuwa na Deo Kihihunga pamoja na Gaitani Sambaya wote wakiwa ni wakazi wa Maguvani katika Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoa wa Njombe.
Pia Diwani wa Kata ya Kitisi Nevi Sanga ,ambapo tukio limetokea katika Kata yake ya Kitisi Mjini Makambako amekili kutokea kwa tukio hilo na kuwachimbaji wa visima wawe makini wakati wa kufanya kazi zilizokuwa zimefanywa na kuachwa kwa muda mrefu kwani Visima vingi ambavyo havitumiki vina kuwa na hewa pamoja na gesi ambapo ukiingia haraka utapata madhara
Baadhi ya Mashuhuda wamesema kuwa kukwama kwa vijana hao kwenye kisima hicho kumesababishwa na kuwa na hewa aina ya kabonidayokisadi .

No comments
Post a Comment