Wafanyabiashara kusamehewa adhabu ya riba na madeni ya kodi .
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya mapato Tanzania imetangaza kusamehe riba na adhabu ya madeni ya kodi kwa wafanyabiashara .
Aidha TRA imetangaza msamaha huo baada ya mkutano kufanyika kati ya Rais ,John Pombe Magufuli pa moja na baraza la wafanyabiashara uliofanyika.Machi 20 ,2018.
Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania [TRA] Julai 11 Mwaka huu imesema msamaha huu umetokana na malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma yakiwa ni riba pamoja na adhabu.
Ikiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya marekebisho kupitia sheria ya fedha ya 2018 na sehemu ya sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015.kulingana na marekebisho yaliyofanyika Waziri Mwenye dhamana ya fedha na mipango amepewa mamlaka ya kutoa msamaha maalumu wa riba na adhabu kwenye malimbikizo kodi kwa silimia 100.Tofauti na asilimia ya awali ambayo ilkuwa asilimia 50.
Madhumuni ya msamaha huo ni kuwapa unafuu wafanyabiashara walipakodi wenye malimbikizo ya riba na adhabu ili waweze kulipa made ya msingi ya kodi kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha 2018 /2019na kuwapa motisha ya kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.
Kulingana na taarifa iliyotolewa imetaja kodi zitakazohusika na msamaha kuwa ni zile zinazotozwa kwa mjibu wa sheria za TRA , isipokuwa ushuru wa forodha unaosimamiwa na sheria ya ushuru wa forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki .

No comments
Post a Comment