Header Ads

Header ADS

Waziri aagiza Mkandarasi kuchunguzwa .

        Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa  ameagiza mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Manga uliopo Wilaya ya Mpanda Mjini Mkoani Katavi achunguzwe na TAKUKURU, kutokana na kutomia mabomba yasiyokidhi viwango.














       
Akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya uongozi wa Mkoa mara baada ya kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji miradi ya maji mkoani katavi .Wakati mradi wa Manga wenye thamani wa shilingi milioni 575 ,unaosimamiwa na Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Mjini Mpanda [MUWASA] na kutekelezwa na Makandarasi  anayejulikana kama Nyalinga Investment Com Ltd  ,uligunduliwa kuwa na kazoro ya mabomba  mara baada ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Mji wa Mpanda  [MUWASA] Mhandisi Zacharia Nyanda kubaini ubovu wa mabomba hayo  na kuyapeleka shirika la viwango vya ubora Tanzania [TBS] kwaajili ya kupimwa na kuonekana hayana viwango .
         Pia amesema kuwa TBS ,imeonyesha kuwa kunatofauti kubwa ya vipimo vya mabomba yaliyotumika  na vipimo vinavyoonekana kwenye mkataba ,hivyo kuthibitisha udanganyifu wa Mkandarasi huyo na kumpongeza Mhandisi Nyanda kwa kugundua mapungufu hayo.
     Mbarawa amesikika akisema kuwa  "Nataka TAKUKURU ,wafanye uchunguzi Mkandarsi huyo alipateje kazi wakati hana uwezo ,na kama kuna mtu kutoka Wizarani anahusika kwa namna yoyote katika jambo hili siku zake zinahesabika maana nitamchukulia hatua mara moja"
      Hata hivyo amesema kuwa atamripoti Mkandarasi huyo kwenye Bodi ya Wakandarasi nchini [CRB] ili wa mchukulie hatua na kutaka asipewe tena kazi zozote za miradi ya maji ,maana Wizara yake haitaruhusu wakandarasi wasio na uwezo kula kodi za wananchi na huku wanaendelea kukosa huduma ya maji safi na salama.
     Pia amesema kuwa atahakikisha changamoto zote zinazokabili ujenzi mradi huu zinafanyiwa ufumbuzi haraka sana   ili mradi huo unao gharimu kiasi cha Dola za kimarekani Milioni 268.35 ambazo zilitokana na Mkopo  nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Exim Benk ,na kukamilika ifikapo Novemba 2019 Badala ya mwaka 2020 kulingana na mkataba.








maamammhuduma ya maji safi na salama 
       

No comments

Powered by Blogger.