Header Ads

Header ADS

Chama kikuu cha Upinzani nchini Chadema kimezindua mafunzo ya Chadema ni msingi.

                    Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema  kimewataka Madiwani pamoja na Wabunge wake kuhakikisha wanaheshimu taratibu na kufuata kanuni za chama hicho ikiwa ni pamoja na kuvaa sare za chama hicho wakati wakiwa kwenye mikutano ya chama hicho.
                 Akizungumza katibu Naibu Mkuu Zanzibar Salimu Mwalimu katika Mkutano uliofanyika Makambako Mkoani Njombe katika Ukumbi wa Mid towan  Hotel Makambako wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya Chadema ni msingi kanda ya Nyasa.
         Viongozi waandamizi wa kitaifa akiwemo Naibu Katibu Mkuu Zanzibar  Salimu Mwalimu wamehudhuria katika Mkutano huo uliokuwa na lengo kuu moja kufungua mafuzo ya Chadema ni Msingi Kanda ya Nyasa.Pia Mwalimu amewapongeza wanachama pamoja na viongoziongozi wa Chama hicho kwa kuweza kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo.
         Hata hivyo Mwalimu amesema kuwa chama hakitaweza kumvumilia mtu yoyote atakaye kwamisha zoezi hilo la chadema ni msingi na chama kitakuwatayari kumuondoa nyasifa alizonazo kama ni kiongozi na kuachishwa uongozi ndani ya chama kwani kukamilishwa zoezi la Chadema ni Msingi itakuwa ni mwanzo  wa maandalizi ya kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa  2019 na hata uchaguzi mkuu wa 2020.
           Pia chadema wamesema katika uzinduzi huo wa mafunzo ya chadema nimsingi itakayoratibiwa kwa awamu ya kwanza ni Majimbo 23yakiwepo Majimbo manne [4] ya Mkoa ya Njombe ikiwa ni Jimbo la Makambako, Jimbo la Njombe ,Jimbo la Makete pamoja na Jimbo la Lupembe.Mkoa wa Iringa majimbo yatakayopitiwa kwa awamu hii ya kwanza ni Iringa Mjini ,Ismani, Kilolo na,Mafinga .Mkoa wa Mbeya majimbo yatakayopitiwa na awamu hii ni Jimbo la Mbalali ,Mbeya Mjini ,Busekelo ,Rungwe ,Mbeya Vijijini na Kyela .Mkoa wa Songwe Majimbo yatakaye pitiwa ni Tunduma ,Songwe ,Momba na mengineyo ya nyanda za kati na kasikazini .Pia Chadema wametaja sasabu zilizo wafanya kuweka kuwa kipaumbele kuwa ni kutokana na matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 kuwa yalikuwa na wapiga kura wengi zaidi ukilinganisha na majimbo mengine.
      Salimu Mwalimu ametumia muda huo kuukosoa mswaada wa manadiliko ya sheria ya Vyama vya Siasa kuwa hauna malengo ya kuendeleza Vyama vya Siasa na badala yake umelengo kuuwa Vyama vya Siasa ha Vya upinzani,na amesema kama chama kinapinga kwa juhudi zote na kuwataka Viongozi wa asasi mbalimbali pamoja na madhehebu mbalimbali ya kidini kuhakikisha wanaupinga mswada huo.Pia Salimu Mwalimu amewataka Viongozi wa Chama hicho pamoja na wanachama kiujumla kuhakikisha wanawapokea vyema viongozi waliopangwa kwaajili ya kuratibu zoezi hilo la chadema ni msingi na kuwapa ushirikiano pindi wakiwa katika maeneo yao.,Ni matumaini yangu kwa  viongozi na wanachama kuwa mtawapokea na kuwa pa ushirikiano viongozi pindi wakiwa katika majukumu yao ya kikazi katika maeneo yenu,Alisema Salimu Mwalimu" Na asitokee mtu yeyote wa kukwamisha kazi hii alisema" Kuweni na upendo pamoja na ushirikiano".
     Viongozi wa Kitaifa pamoja na Kanda bado wanaendelea na ziara ya mafunzo ya Chadema ni Msingi kanda ya Nyasa katika Mkoa wa Njombe.

    Mwandishi
                    Mwita George Kihungu












No comments

Powered by Blogger.