Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Makambako Kata ya kitisi kimewataka viongozi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi linaloendelea la uandikishaji wa Chadema ni Msingi.
Chama cha Chadema kimewataka Viongozi wote wa Chama na wanachama kiujumla kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji wa chadema ni msingi.
Hayo yamesemwa katika kikao cha dharura kilichofanyika katika kata ya Kitisi Chadema na Diwani wa Kata ya Mwakibete Mkoani Mbeya Lukas Mwampiki ambaye ndiye msimamizi katika zoezi la uandikishaji wa Chadema ni msingi katika Jimbo la Makambako.
Pia Mwapiki ,ametumia fursa hiyo kuwaambia wanachama na viongozi kuwa wahakikishe wanajiandaa vyema katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotegemea kuanza mwaka huu 2019.Kiongozi huyo amesemakuwa chama kimejipanga vyema na kuhakikisha kinatoa wagombea wanaokubalika katika jamii na kuweza kuibuka washindi katika chaguzi za serikali za mitaa.
Kwa upande wake Katibu wa kata kitisi GEORGE KIHUNGU MWITA, Amesema kuwa atahakikisha anahamasisha wanachama wote wa kata hiyo kuhakikisha wanajiandikisha katika vitabu vilivyo andaliwa kwa ajili ya uandikishaji wa zoezi la chadema ni msingi.Akizungumza na mtandao huu amesema kuwa atahakikisha zoezi hili lazima likamilike .
Zoezi la uandikishwaji wa Chadema ni Msingi lilianza toka tarehe 16.12.2018 na bado linaendelea kufanyika katika kata zote na mitaa yote ya Jimbo la Makambako Mkoani Njombe.
Hayo yamesemwa katika kikao cha dharura kilichofanyika katika kata ya Kitisi Chadema na Diwani wa Kata ya Mwakibete Mkoani Mbeya Lukas Mwampiki ambaye ndiye msimamizi katika zoezi la uandikishaji wa Chadema ni msingi katika Jimbo la Makambako.
Kwa upande wake Katibu wa kata kitisi GEORGE KIHUNGU MWITA, Amesema kuwa atahakikisha anahamasisha wanachama wote wa kata hiyo kuhakikisha wanajiandikisha katika vitabu vilivyo andaliwa kwa ajili ya uandikishaji wa zoezi la chadema ni msingi.Akizungumza na mtandao huu amesema kuwa atahakikisha zoezi hili lazima likamilike .
Zoezi la uandikishwaji wa Chadema ni Msingi lilianza toka tarehe 16.12.2018 na bado linaendelea kufanyika katika kata zote na mitaa yote ya Jimbo la Makambako Mkoani Njombe.
No comments
Post a Comment