Kanisa katoliki latoa msaada wa vifaa katika Magereza ya Mkoa wa Njombe
Kanisa Katoliki lachangia vifaa vya Magereza mkoa wa Njombe
Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe
limetoa msaada wa vifaa vya ofisi kwa ajili ya ofisi ya Mkuu wa Magereza
mkoa wa Njombe vyenye thamani ya zaidi ya Milioni mbili, kwa lengo la
kuunga mkono juhudi za jeshi hilo za kurekebisha tabia za wahalifu
katika jamii ya wakazi wa mkoa huo.
Akizungumza kwa niaba ya Askofu wa jimbo
hilo, Alferd Maluma Katibu wa askofu, Innocent Chaula, amesema kuwa
Kanisa kama mdau wa kurekebisha tabia kiroho linafurahi kuona jeshi hilo
pia likijitahidi kuwaongoza wanajamii walioteleza kurudi katika matendo
ya kimaadili hali ambayo inawajengea heshima.
‘’Mimi nimetumwa na baba Askofu Maluma
kuleta vifaa kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya magereza Mkoa na
tumefanya panapo wezekana nimeleta Viti vya kukalia Sita, Kompyuta ya
mezani moja, na simu za upepo’’amesema Chaula.
Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Njombe, Festo Ng’umbi, amelishukuru Kanisa hilo na kutumia fursa hiyo
kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuchangia ujenzi wa ofisi ya mkoa huo
ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
No comments
Post a Comment