Header Ads

Header ADS

Serikali ya Mkoa wa Njombe ya charuka juu ya Utekwaji na mauaji ya watoto.

           Wakati wananchi wa Mkoa wa Njombe wakiwa katika majonzi makubwa yanayotokana na utekwaji pamoja na mauaji ya watoto yanayojitokeza mkoani humo .Serikali ya Mkoa imelaani vikali juu ya matukio hayo .
        Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Polisi Mjini makambako.
  " Wenyeviti wa Mitaa,Wenye viti wa Vijiji na Waheshimiwa Madiwani mtoe ushirikiano wa kwanza kwa vyombo vyangu vya ulinzi na usalama juu ya utoaji wa taarifa za matukio ya utekwaji na mauaji ya watoto "Alisema Ole Sendeka.
     "Kwanzia sasa akifariki mtu mmoja , akiuawa mtu mmoja kwenye mtaa huo na halafu mkatuambia ameuawa na watu wasiojulikana naanza na mwenyekiti wa mtaa huo ,Naanza na mwenyekiti wa kijiji hicho na mtendaji wa kijiji hicho nao wataunganishwa kwenye kesi ya mauaji mpaka watakaposhiriki kuwataja wahalifu hao" Alisema Olesendeka.

              Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ,Amewatahadharisha wananchi juu ya matapeli watakaojitokeza na kujifanya maafisa usalama wa Taifa ."Natoa onyo kali sana kwa matapeli watakaojivalisha kofia kujifanya kuwa wao wapo pamoja nasisi kwenye timu natoa onyo kali sana tukimpata mmoja wapo natakanikuambie tutamsahau na ajisahau " alisema Ruth Msafiri.
                 Itakumbukwa kuwa mpaka sasa imefikia idadi ya watoto  sita [6] waliofariki kwa matukio ya utekwaji na mauaji hayo na watoto wanne [4] wamenusurika kuuawa na kuokolewa wakiwa hai.

No comments

Powered by Blogger.