Mtoto mwingine Njombe akutwa amefariki
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa baba mzazi wa mtoto Rachael Malekela (7) ambaye alikutwa ameuawa jana usiku katika Kijiji cha Kata ya Matembwe Wilayani Njombe.
Wakati Serikali ikichukua jukumu la kuthibiti matukio ya utekwaji na mauaji ya watoto Mkoani Njombe bado wimbi hilo linazidi kuongezeka Mkoani Njombe .Baada ya kuokotwa maiti nyingini vichakani ya mtoto mwenye umri wa miaka 7 .Aliyejulikana kwa jina la Rachel Malekela ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Matembwe iliyopo Wilaya ya Njombe na Mwili wake kutupwa kichakani.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kijiji cha Matembwe ,Brayson Malekela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa binti huyo ni mtoto wa mdogo wake .Pia amesema kuwa wazazi wa binti huyo walibaini kuwa binti huyo haonekani jana majira ya saa 12 jioni na kutoa taarifa katika uongozi wa kijiji na wananchi wakaanza kumtafuta na saa 4 usiku walikuta mwili wa mtoto huyo katika msitu wa miti mipana uliopo kijijini hapo.
"Huyo mtoto shingoni kama vile amechomwa na vitu vyenye ncha kali pia sehemu ya shingo kwa nyuma kama amechomwa na vitu vyenye ncha kali na kwenye koromeo kama amekatwa hivi "Alisema mwenyekiti wa kijiji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amekili kupata taarifa hizo zinazo husiana na tukio la mauaji hayo na kuahidi kuzitolea ufafanuzi."Ni kweli mtoto kwa jina ndio huyo na ameuawa nyuma tu ya nyumba yao na kutupwa kwenye shamba la miti" Alisema Mkuwa Wilaya.
Endelea kupitia ukurasa wetu kwa habari kamili.
Na mwandishi: GEORGE KIHUNGU MWITA.
No comments
Post a Comment