Watano wauawa Njombe kisa mauji ya watoto
Kufuatia vifo vya watoto 6 mkoani Njombe, watoto 3 wakiwa kutoka
familia moja wenye umri wa miaka chini ya 10, Mkuu wa Mkoa wa Njombe
Christopher Ole Sendeka amesema kuwa watu watano wameuawa na wengine
watatu kujeruhiwa vibaya na wananchi baada ya kushukiwa kuhusika na
mauaji ya watoto.
Tukio hilo limetokea siku ya jana katika wilaya za Njombe na Wanging’ombe.
Huku vyombo vya dola vikiendelea na sakasaka la wauwaji wa watoto hao waganga wa kienyeji mkoani humo wametakiwa kusitisha kwa muda shughuli zao wakati huu ambapo operesheni maalumu inaedelea mkoani humo kubaini chanzo halisi na wahusika wa mauaji hayo.
Kwani watoto hao walikutwa katika mazingira ya kukutatanisha ikiwa pamoja na baadhi ya viungo vya miili yao kuwa vimenyofolewa pamoja na macho, meno na sehemu za siri, hali iliyopelekea mauaji hayo kuhusihwa na ushirikina
Aidha, katika kikao kilichofanywa na waganga wa kienyeji na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni wilayani Njombe waganga wa jadi wamesema wao si chanzo cha tatizo na kuitaka serikali ifanye uchunguzi zaidi
Kiongozi wa waganga wa tiba za jadi Antony Mwandulami amedai kuwa watu wamekuwa wakilipiziana visasi kwa mauaji na kusingiziwa waganga wa jadi.
“Kuna mambo mengi nyuma ya haya mauaji. Wapo ambao wanalipiziana visasi na hawaonekani lakini waganga wanalaumiwa kwa kusemwa kuwa wapiga ramli chonganishi,” Amesema Mwandulami.

No comments
Post a Comment