Wazazi wakubaliana kuwa mzazi atakayemshawishi mwanafunzi kufanya vibaya mitihani yake hususani ya kumaliza elimu ya darasa la saba hatua kali zichukuliwe.
Wananchi wa kata ya Kitandililo Halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe, wameazimia kuwa mzazi au mlezi atakae mshawishi mwanae afanye vibaya katika masomo yake hususani katika mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi hatua za Kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Licha ya kuamua mzazi huyo ashughulikiwe kisheria pia wananchi hao wamekubaliana kuwa muhusika apewe adhabu ya kumsomesha mtoto wake katika Shule ya Sekondari Mtwango ambayo ni shule binafsi, ili kukabiliana na gharama zilizopo katika Shule hiyo tofauti na Shule za Serikali.
Wananchi hao mbele ya Diwani wa Kata ya Kitandililo, Imani Fute wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakaye onekana amesimama na mwanafunzi wa kike kwa zaidi ya dakika tano atakabiliwa na adhabu ya kununua mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari ya kata hiyo.
“Ukimpenda Mwanafunzi ukubali kuchangia mifuko kumi ya saruji ili ajengewe mabweni apate kusoma kiurahisi zaidi kwa kutokutembea umbali mrefu”. Wameeleza Wananchi hao.
No comments
Post a Comment