Maandamano sudani yasababisha shule kufungwa
Kutokana na maandamano yaliyoibuka baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano katika Jimbo la Kordofani Mamlaka ya utawala wa Kijeshi nchini Sudani imeamuru masomo kusimamishwa na shule kufungwa nchi nzima.
Pia maandamano hayo yalilenga katika malalamiko kwenye sekta ya mafuta na upungufu wa mkate ikiwa wanafunzi wanne na mwananchi mmoja wameripotiwa kupoteza maisha ,watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya risasi kufyatuliwa kiholela.
Kutokana na taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Suna mamia ya wanafunzi waliovalia sare za shule waliandamana wakiwa wanapunga bendera za Nchi yao kudai haki ya wenzao waliouawa na kupelekea mamlaka kuamuru Magavana wa Majimbo yote kufunga shule zote mpaka yatakapotolewa maelezo mengine.

No comments
Post a Comment