Header Ads

Header ADS

Chadema wakalia kidedea kesi ya kuvuliwa Ubunge kwa Tundulisu

      Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimesema kuwa wao kama Chama ndio wadhamini wa kubwa wa Ubunge wa Tundulisu kwani hawezi kuwa Mbunge bila kuwa Mwanachama.Hayo yamesemwa na katibu Mkuu wa Chama hicho Dr .Vicent Mashinji Jijini Dare s Salaam.Baada ya kusogezwa mbele kesi ya maombi iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundulisu.









   Dr,Mashinji amesema kuwa kitendo cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Job Ndugai kumvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Tundulisu umekiathiri Chama hicho.








        Kama mnavyojua Katiba ya Nchi inavyosema huwezi kugombea cheo chochote cha Serikali kama kama hujadhaminiwa na Chama cha Siasa ,kwa hiyo Lisu anatokana na Chadema kwa hiyo kuvuliwa Ubunge wake ni maamuzi ambayo yamekiathiri Chama"Hivyo na sisi tutasimama naye bega kwa bega ,Tukutane Agost 23 siku itakapo somwa tena kesi yake"Amesema Dr. Mashinji.
          Pia mdogo wake Tundulisu  Vicent Mughwai amesema kuwa wao kama familia wapo pamoja na ndugu yao ambaye hajarudi nchini kutokana na kuendelea na matibabu nchini Ubelgiji  na kusema kuwa anawashukuru watanzania ,waandishi wa habari na wanaoendelea kuomba ili haki iweze kutendeka katika shauri hilo lililofunguliwa mahakamani hapo.
         Na kuhusu kurudi nyumbani kwa Tundulisu Mughwai amewataka Watanzania kuwa wavumilivu ambapo muda ukifika kila kitu kitawekwa wazi kuhusu ujio wake lakini akasema kitu cha msingi ni Ubunge wake.

No comments

Powered by Blogger.