Wakurugenzi 40 watiwa mashakani na kuitaji wajieleze kwanini hatua dhidi yao zisichukuliwe
Suleiman Jafo,ambaye ni Waziri wa Nchi,ofisi ya Rais,Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa[TAMISEMI] atoa muda wa siku 14 kwa wakurugenzi wa halimashauri zaidi ya 40 Nchini kurejesha barua za kujieleza kwa nini hatua dhidi yao isichukuliwe kwa kupereka asilimia 10 ya wanawake,vijana na walemavu chini ya asilimia 50 ya mapato yao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ameeleza kwamba wakurugenzi hao wa halimashauri wanaitajika kuandika barua kwenda kwa katibu mkuu wa TAMISEMI ndani ya wiki mbili wakijieleza kwa nini hatua dhidi yao ya uvunjifu wa sheria zisichukuliwe.
Lakini pia katika halimashauri zilizofanya vibaya katika ukusanyaji wa mapato chini ya asilimia 50 ya malengo waliyojiwekea agizo hilo linawahusu.
Hata hivyo,Jafo ametoa pongezi katika Majiji 6 kwa ukusanyaji mzuri wa mapato wakiongozwa na Jiji la Arusha ambalo lilikusanya asilimia 105 huku Jiji la Dodoma likiongoza kwa shilingi bilioni 71.727 kama pato ghafi.
Jafo ameeleza kuwa kukusanya ni jambo moja na kuhakikisha mapato yanaenda kwa wananchi kupitia miradi na ni jambo la pili na hivo kulitaja Jiji la Dodoma pekee kupereka asilimia 75 ya mapato yake kwa wananchi.
Vilevile,ameeleza kuwa kwa upande wa halimashauri zote zilizofanya vibaya kwa ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019 zawadi ya vinyago itatolewa dhidi yao.

No comments
Post a Comment