Header Ads

Header ADS

kesi ya Lissu kuanza leo

  Tundu Lissu aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki kwa tikeki ya chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA]kupitia kwa wakili wake dhidi ya Spika Wa Bunge,Job Ndugai kesi yake inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo katika Mahakama kuu ya Tanzania Masjala kuu ya Dar es salaam.
    Kesi hiyo,ikihusu upingaji wa Lissu dhidi ya maamuzi ya Spika Job Ndugai yakihusu kumvua Ubunge Tundu Lissu juni 28 mwaka huu.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ya Chadema,Tumaini Makene ameeleza kwamba maombi ya kesi hiyo yatasikilizwa mbele ya Jaji Mtupa.











  Makene ameeleza kwamba kulingana na hati ya wito ya Mahakama  inabainisha kuwa mlalamikiwa ambaye ni spika wa Bunge Job Ndugai atalazimika kufika Mahakamani hapo bila kukosa akiwa na nyaraka zote.
   ''Tunatoa wito kwa viongozi,wanachama,wafuasi wa Chadema na watanzania wote wapenda haki, Demokrasia na utawala bora unaoheshimu sheria,mahali popote walipo kufuaatilia kwa karibu shauri hii kuanzia sasa'',Makene ametoa taarifa hiyo.
  Lakini pia,taarifa hiyo imesema kwamba wameamua kwenda mahakamani baada ya Spika Ndugai kutamka kuhusu ukomo wa Mbunge Lissu kwa ajiri ya kufuata haki alipokuwa akiahirisha mkutano wa Bunge la bajeti jijini Dodoma mnamo juni 28 mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.