Header Ads

Header ADS

CPJ ,Yaingilia kati kesi ya Kabendera

            kamati ya kimataifa ya kulinda  Waandishi habari CPJ imeandika barua ya wazi kwa Serikali ya  Tanzania kutaka Serikali kufuta mashitaka dhidi ya Mwandishi wa habari Erick Kabendera na maelezo kuhusu Azory Gwanda.
  Barua hiyo ya wazi kwa Serikali ya Tanzania imeeleza kwamba ni mwezi uliopita tu wakati wa Mkutano wa kutetea uhuru wa vyombo vya habari mjini Landon,Palamagamba Kabuti ambaye ni Waziri wa mambo ya kigeni Tanzania amethibitisha kwamba Serikali yake inataka
''Kuwezesha uandishi habari wa kiuchunguzi''na ''kuhakikisha kwamba Waandishi habari wanalindwa dhidi ya hatua zote,kushitakiwa ama kukamatwa''.Kabendera kumruhusu kurejea katika kazi yake,na kulichukulia kwa kina suala la kupotea kwa Gwanda.Litakuwa ni hatua muhimu kuelekea kutimiza ahadi hizi.











   Julai 29,2019 Kabendera alichukuliwa kwa nguvu kutoka nyumbani kwake,na kutopewa au kunyimwa uwezekano wa kuwakilishwa na wakili kwa zaidi ya masaa 24.Mwanzo vyombo vya Usalama na Ulinzi  vilidai kuwa wanachunguza Uraia wa Kabendera,lakini siku chache mara  baada ya kukamatwa kwake waendesha mashitaka walibadili njia na kumshitaki kwa uhalifu wa kiuchumi,mashitaka ambayo hawezi kupata mzamana.

No comments

Powered by Blogger.