Taarifa kwa UMMA kuhusu kubadili kozi
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI YA UHAMISHO AU KUBADILI KOZI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI YA UHAMISHO AU KUBADILI KOZI
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi katika vyuo vinavyotoa mafunzo kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada ambavyo si vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki nchini.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwafahamisha wahitimu wa Kidato cha Nne 2018 waliopangiwa vyuo na kozi mbalimbali na OR-TAMISEMI kwamba wanaruhusiwa kuomba Uhamisho au Kubadili Kozi kuanzia Tarehe 10 Agosti, 2019 hadi Tarehe 30 Agosti, 2019.
Hivyo waombaji wanatakiwa kuzingatia yafuatao:
- Uhamisho au kubadili kozi unafanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) kwa kubofya UTHIBITISHO/UHAMISHO TAMISEMI na majibu yatapatikana moja kwa moja unapokamilisha uhamisho.
- Uhamisho au kubadili kozi utawezekanakwa wale waliothibitisha tu. Mwombaji ambaye hajathibitisha anashauriwa kufanya hivyo endapo bado nafasi zitakuwa wazi.
- Vyuo au kozi zitakazooneka ni zile tu ambazo zina nafasi.
- Muombaji atalazimika kulipia Ada ya Shilingi Elfu Tano tu kama gharama za uhamisho au kubadili kozi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBUMTENDAJI
BARAZALA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 10/08/2019
OFISI YA KATIBUMTENDAJI
BARAZALA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 10/08/2019
No comments
Post a Comment