Header Ads

Header ADS

Ajali Ya Lori Morogoro,Lugola Atoa Onyo

Kupitia tukio la ajali ya Lori iliyopelekea vifo vya Watanzania zaidi ya 66,Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema Watanzania hawana budi kujifunza.
   Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ameeleza hayo Mkoani Morogoro,amesema kuwa  wananchi hawana budi kuviachia vyombo vya ulinzi na maafa kushughulika masuala hayo wakati ajali kama hizo zinapotokea.










''Tukio hilo sio la kwanza kutokea na kujifunza ila niseme watanzania hatuna budi kujifunza,matukio ya namna hiyo yanapotokea tuviachie vyombo vya usalama na majanga ya ajali viendelee kushughulika,sisi wengine tukae pembeni''.Amesema Lugola
   Hata hivyo,Lugola amesema wao kama Serikali licha ya kukemea wataendelea kufuatilia watu wanaosambaza picha zisizofaa Mtandaoni,Pia amewaomba Watanzania kuendelea kudumisha sheria za Mitandaoni.

No comments

Powered by Blogger.