Watu kumi wanusurika kwenye Bahari ya Hindi,Jijini Tanga.
Baada ya boti kuzama kwenye Bahari ya Hindi watu kumi wanusurika kifo na mmoja kutojulikana alipo wakati wakiwa wameenda kuzuru visiwa vilivyopo majini.
Edward Bukumbe ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoani humo ameripoti tukio hilo lililotokea Agosti 11 ambapo watu hao walikuwa wamepanda boti hiyo waliyokuwa wamekodi eneo la Yanchi Pub.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani humo ameeleza kuwa mara baada ya watu hao kupanda boti hilo kwa lengo la kutembelea visiwa mbalimbali vinavyopatikana katika Bahari hiyo ndipo upepo mkali ulivuma na kuwazuia kwenda mbele pia walipohitaji kugeuza kuweza kurudi
walikotoka ndipo boti hiyo ilipinduka.
''Watu hao walikuwa wametokea eneo la Yanchi club walikuwa wanakwenda kutembelea visiwa mbalimbali vya Bahari ya Hindi wakati wakiwa njiani upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kurudi walipinduka''.Amesema Bukombe
Pia,Bukombe ameeleza kuwa boti hiyo ilikuwa na watu 11 na 10 kati ya hao waliokolewa kutokana naq kuvaa maboya yaliyokuwemo kwenye boti hiyo na mmoja wao mwingine hakuwa nalo na kupotea na inasemekana mpaka sasa haieleweki alipo.
''Natoa wito kwa wananchi wanaotumia Bahari kusafiria kuchukua tahadhari wanapokuwa Baharini kwa kuhakikisha wanavaa maboya ya kujiokolea ili wakati yanapotokea majanga kama hayo waweze kuona namna ya kujiokoa''.Amesisitiza Bukombe.

No comments
Post a Comment