Header Ads

Header ADS

Jafo awajibu Chadema Suala la Watendaji kuitwa Ikulu

Hatua ya kuitwa kwa Watendaji Kata ambao wametakiwa kufika Ikulu jijini Dar es Salaam ifikapo Septemba 2,2019 Imeshangazwa na Makada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema,John Mlema Akizungumza na kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio amesema kuwa hana wasiwasi na kitendo hicho cha kuitwa kwa Watendaji Ikulu.
  "Kitendo cha Serikali kuwaita Watendaji wa Ngazi ya chini  kabisa hakijawahi kutokea  kwenye Nchi yetu,Tulitegemea kama kuna maagizo yangeweza kutoka TAMISEMI,hadi chini,Kiendo cha Serikali kuu kuwaita Watendaji maana yake Watendaji TAMISEMI wameshindwa".Amesema John Mlema.











Aidha Jafo wakati akijibu madai hayo, ameeleza kushangazwa kwa namna ya jambo hilo lilivyopokelewa kwa namna ya kisiasa.
  "Ni jambo la ajabu sana kama kila jambo wanataka kulipeleka kisiaasa,taifa haliwezi kwenda mbele,watu tuko kazini nadhani kila kitu kikitafsiriwa kisiasa nadhani tutakuwa hatuitendei haki Tanzania yetu,watu wawaache Viongozi wa Serikali wafanye kazi".Ameeleza Jafo.
    Pia,hivi karibuni kumesambaa Barua ikionyesha kuitwa kwa Watendaji kata Nchini kote ambao watakutana na Rais Septemba 02,Mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.