Kesi ya vigogo wa Chadema watumika rasmi mahakamani ushahidi wa video
Ushahidi katika kesi inayowakabili viongozi sita wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe imewasilishwa rasmi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa njia ya video Mahakamani na shahidi wa sita kama kama ushahidi katika kesi hiyo.
Ni muda zaid ya mwaka mmoja na nusu tokea kesi hiyo inayowakabili Viongozi hao wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ni ya uchochezi.
Mnamo Machi 27,2018 Mbowe na viongozi wengine wanane wa Chadema walifikishwa Mahakamani wakikabiliwa na mashtaka manane kwa mara ya kwanza.
Dkt.Vincent Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama hicho,John Mnyika pia ambaye ni Naibu Katibu Mkuu bara pamoja na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalim,hao ni Viongozi wengine walioshtakiwa mbali na Mbowe.
Hata hivo viongozi wengine ambao walishtikiwa ni Ester Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini,John Heche Mbunge wa Tarime Vijijini,Ester Mtiko Mbunge wa Tarime Mjini,Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini pamoja na Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kawe.
Mara kadhaa toka Februari 2018 ulipofanyika uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kinondoni baada ya kudaiwa kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali ambayo yalitawanywa na Polisi,Vigogo hao walikuwa wakiojiwa na Polisi kabla ya kufikishwa Mahakamani.

No comments
Post a Comment