Header Ads

Header ADS

Ombi la Marekani la kuzuia Meli ya Iran lakataliwa na Gibraltar;Mgogoro wa Meli ya Mafuta Iran

Gibraltar imepinga tena ombi la Marekani kuikamata meli ya mafuta ya Iran ambayo ilikua ikiizuia tangu mwezi julai ikidhania kwamba ilikuwa ikisafirisha mafuta ya Syria.
  Ombi hilo lilipelekwa na Marekani siku ya ijumaa,siku moja baada ya Gibraltar kuachia meli hiyo ya Grace 1.
   Gibraltar imesema haikuwa tayari kukubali la Marekani kuikamata tena meli hiyo kwa kuwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havina nguvu.
  Tayari meli hiyo imeondoka Gibraltar kulingana na mjumbe wa Iran nchini Uingereza.











Tehran imeeleza kuwa  ipo tayari kuyapeleka majeshi yake kuisindikiza meli hiyo ya Adrian drya1 ambalo jina hilo lilibadilishwa kutoka jina la awali Grace1
 Aidha meli hiyo pamoja na wafanyakazi wake 29 kutoka India,Urusi,Latvia na Ufilipino ilikamatwa kuputia msaada wa wanamaji Uingereza tarehe 4 julai baada ya Serikali ya Gibraltar eneo lililochini ya Uingereza kusema kuwa ikielekea Syria hatua inayokiuka vikwazo vya Muungano wa Ulaya.
  Hata hivyo jambo hilo limezua mgogoro wa kidiplomasia baina ya Uingereza na Iran ambao bado umeendelea kwa wiki za hivi karibuni huku Iran nayo ikilipiza kwa kuikamata Meli iliyokuwa ikipepea bendera ya Uingereza Stena  Impero katika Ghuba.

No comments

Powered by Blogger.