Header Ads

Header ADS

Mwanaharakati nchini Uganda afungwa jera miezi 18

          Mwanaharakati Dk .Stella Nyanzi amehukumiwa kwenda jera kifungo cha miezi 18 kwa kupatikana na kosa la unyanyasaji wa kimtandao pamoja na mawasiliano ya udhalilishaji dhidi ya Raisi Yoweri Mseveni na familia yake.











      Mwanaharakati huyo alikataa kumsikiliza hakimu akisoma hukumu  dhidi yake na badala yake akafanya vurugu kwa kuvua nguo na kuonyesha sehemu za mwili wake.
       Dkt .Nyanzi hakuwa mahakamani lakini hukumu dhidi yake ikatolewa kupitia video link  kutoka Jela .Wakati kesi ikiendelea B.Stella  alikataa kuomba dhamana  na kuwa katika gereza kuu  la Uganda la Luzira kwa muda wa miezi minane.Kwa mjibu wa mahakama ya uganda mwanaharakati huyo sasa atazuiliwa gerezani kwa  zaidi ya miezi tisa.
      Mwanaharakati huyo alikuwa ni mtafiti wa maswala ya jamii na ni msomi na kabla ya kuanza kampeni yake ya matusi kupitia mitandao ya kijamii alikuwa ni mwalimu wa chuo kikuu cha umma nchini Uganda cha Makerere.

No comments

Powered by Blogger.