Header Ads

Header ADS

Ndugai aeleza kuwa hategemei kuona rushwa ikitawala kwenye uchaguzi

 Job Ndugai ambaye ni Spika wa Bunge amesema kuwa kipindi cha uchaguzi hategemei kuona vitendo vya rushwa vikiendelea na juhudi kubwa sana iliyofanywa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika kukomesha vitendo vya Rushwa Nchin.
     Hayo ameeleza wakati akiwa kwenye kongamano la kumpongeza Rais Magufuli lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Nchini Tanzania UWT lililofanyika Mkoani Kirimanjaro akiwakilishwa na Naibu Spika Tulia Ackson.











''Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi[CCM] ya mwaka 2015-2020,imetekelezwa kwa kiwangu kikubwa na kwamba miongoni mwa mambo ambayo ametekereza Rais ni kurejesha nidhamu kwa watumishi,na kwa kazi kubwa aliyoifanya hatutaona Rushwa kwenye chaguzi zijazo''.Hayo yamesemwa na Ndugai.
      Lakini pia,Naibu Spika ameeleza kwamba hali kubwa ambayo itapelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa Rushwa ya uchaguzi katika chaguzi zijazo ni pamoja na kushughulikia tatizo sugu la rushwa ndani ya Serikali pia ndani ya Chama Cha Mapinduzi[CCM}.

No comments

Powered by Blogger.