Baraza JIpya la Mawaziri latangazwa Rasmi na Rais Tshsekedi,Kinshasa
Hatimaye baada ya kusuburiwa kwa muda wa miezi saba,Serikali ya Kwanza ya Rais Felix Tshisekedi imetangaza leo Baraza la Mawaziri,Kinshasa Katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wanawake wamepewa asilimia kumi na saba ya Mawaziri na Wanaume wamepewa asilimia themanini na tatu katika Serikali hiyo mpya.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa BBC Mjini Kinshasa anasema Katika Baraza hilo Jipya la Mawaziri kuna Sura Mpya hazijawahi kuonekana katika Serikali.
Hata hivo Wizara maalumu imeundwa ambayo itashughulikia masuala ya Ulemavu.
Nchini DRC Congo Serikali inajukumu la kuboresha na kuimarisha usalama wa raia wake.
"Serikali hatimaye imewadia.Rais amesaini agizo rasmi na tutaanza kufanya kazi hivi karibuni".Waziri Mkuu Sylveste Illunga amenukuliwa na Shirika la Habari la AFP.
Felix Tshisekedi ambaye ni Rais wa DRC Congo Pamoja na Mtangulizi wake Joseph Kabila walikubaliana kuunda Serikali ya Muungano,Mnamo julai mwaka huu.
Makubaliano yao ilikuwa ni kuunda Serikali itakayo kuwa na Mawaziri 66.
Kulingana na Makubaliano yao Felix Tshisekedi amejinyakulia Wizara 23 ambapo chama cha rais wa zamani kimelijipatia wizara 43.
Wakati maswali yakiulizwa kulikua na madai kwamba Bwana Tshisekedi alifanya makubaliano ya kugawana madaraka na Bwana Joseph Kabila kabla ya Uchaguzi kufanyika.
Serikali itatangazwa baada ya mashauliano kumalizika baina ya vyama vyao na pande hizo mbili.
Sura mpya hiyo ya Mawaziri imetangazwa rasmi Kinshasa,baada ya miezi saba kupita.
No comments
Post a Comment