Header Ads

Header ADS

Afungwa Maisha kwa unyanyasaji wa Kingono.

Shirika la Habari la Dallas News,limetoa taarifa za raia mmoja wa Kenya ambaye anadaiwa kumnyanyasa kingono ajuza wa Miaka 74.
Pia hatua hiyo inakuja baada ya raia mwingine wa Kenya kuwaua wazee  11 mjini Texas miezi kadhaa iliyopita.
Mtuhumiwa wa kosa hilo Anthony Mamboleo anadaiwa kutekeleza tukio hilo Januari 2018 la kumbaka Ajuza wa miaka 74 ambaye alikuwa ni mgonjwa.
"Muuguzi aliyekuwa anamuudumia ajuza huyo alimpata anatokwa na damu sehemu za siri.Uchunguzi umeonyesha muathiriwa alikuwa anadhulumiwa kingono mara kwa mara.Huku uchunguzi wa chembechembe za vinasaba uliofanyiwa na wahudumu wote ukilingana na wa Nyakeo''.Mwendesha mashtaka aliliambia Shirika la habari la Dallas.
  Nyakeo,alikuwa akihudumu kama Muuguzi katika kituo cha Afya cha Woodridge ambacho kinatoa huduma ya kuwarekebisha watu tabia mjini Grapevine.
Ajuza huyo alikuwa akiugulia na ugonjwa wa (Elzhema)unaosababisha kupoteza kumbukumbu.Alifariki baadae mwaka huo.











Kesi hiyo ilipokuwa inasukilizwa,Mahakama ilifahamishwa kuwa Nyakeo alifanya tukio hilo pindi muathiriwa wake akiwa hana uwezo wa kukataa au kukubali kitendo hicho kutokana na ugonjwa huo wa akili.
 ''Hakuwa na uwezo wa kuzungumza,kujilisha wala kujipeleka msalani na alikuwa akivishwa Diaper na wauguzi''.Jordan Rolfe,mmoja wa maendesha mashtaka aliiambia mahakama.
Mashtaka hayo yalikanushwa na Bw.Nyakeo akidai kwamba kuna mtu alitumia DNA kutoka kwenye mpira wa kondomu uliotumika na kumwekea mama huyo.
  "Nilimuogesha tu na kumpeleka kwenye eneo la chakula".Alisema Nyakeo.
Mfanyakazi mwenzake alietoa ushaidi wa tukio hilo anasema alipoona hali ya mwathiriwa moja kwa moja alihisi kunyanyaswa kingono kwa mgonjwa huyo.
 "Hiki si kitendo kinachofanywa kila siku hususani na wanawake wazee walio katika umri huo,kwa ufahamu wangu".Alisema
Pia waendesha mashtaka walidai Nyakeo alishawahi kuwanyanyasa kimapenzi wafanyakazi wenzake na kwamba wakati wa uchunguzi alijaribu kutoroka Texas.
"Alimwambia rafiki na mfanyakazi wa zamani kudanganya kwa niaba yake wakati wa kutoa ushahidi''.walinukuliwa katika nyaraka hizo.
Jordan Rolfe aliwaambia majaji kuwa Nyakeo anastahili kufungwa kwa kufanya kitendo hicho cha kiajabu,Alisema hayo katika hoja ya kukamilisha kesi.

No comments

Powered by Blogger.