Tarehe ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 yawekwa wazi.
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa Selemani Jafo ameweka wazi tarehe rasimi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019.
Ameyasema hayo Dodoma leo tarehe 23 Agosti 2019 wakati akitoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa na viongozi mbalimbali kuelekea uchaguzi huo.
Jafo ,amesema kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa Utafanyika tarehe 24 Novemba 2019 na zoezi la kupiga kura litaanza saa mbili kamili asubuhi mpaka saa kumi kamili jioni.Pia amesema kuwa kampeni za uchaguzi zitafanyika siku saba kabla ya siku ya kuanza uchaguzi na kila chama kitakachoshiriki katika uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya kampeni si chini ya siku saba kabla ya kampeni kuanza.
" Ofisi ya Mkoa ndiyo itakuwa mratibu mkuu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mkoa husika ambapo Halmashauri za Wilaya zitawajibika kuratibu uchaguzi kwa mjibu wa maelezo yaliyoonyeshwa katika muongozo kwa mujibu wa kanuni hizi viongozi waliochaguliwa katika Serikali za Mitaa uliopita ukomo wa uongozi wao ni siku 7 kabla ya siku ya kuchukua fomu kuanza kampeni "Amesema Jafo

No comments
Post a Comment