Header Ads

Header ADS

Wanufaika wa NASAF ,Wadai wapatiwe fedha.

             Katika Vitongoji sita vya kijiji Wanginyi Wilayani Njombe wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini Tanzania TASAF .Wamemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwapa ufafanuzi kwanini hawajapatiwa fedha hizo tangu kuanza kwa mwaka huu wakati maeneo mengine yameendelea kunufaika na mpango huu wa TASAF.











  Hayo yamesemwa katika mkutano wa hadhara mbele ya Mbunge wa Jimbo la Lupembe ,Joram Hongoli wanufaika wa TASAF.akiwemo Samuel  Ngimbuchi wamesema kuwa hali yao imezidi kuwa ngumu kwa kuwa idadi kubwa ya wazee  na familia duni zimekuwa zikitegemea fedha hiyo kuendeleza miradi ya ufugaji na kilimo pamoja na maisha yao ya kila siku na kuiomba serikali kutafutia majibu changamoto hiyo.
    Pia wanufaika hao wamelalamikia utaratibu uliotumika awali kuainisha kaya zenye uhitaji wa mfuko kwa kuwa wazee wengi wenye sifa  pamoja na kaya duni huku baadhi ya wasiyo na sifa wakionekana kunufaika na mpango huu wa TASAF ,jamba ambalo wanaliona kuwa liligubikwa na upendeleo na kuiomba serikali kurudia tena mchakato wa kuwapata wanufaika hao.
      Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Wanginyi Emanuel Mwenda anakanusha tuhuma hizo za kugubikwa kwa upendeleo kwa waratibu wa TASAF ,huku akisema kuwa idadi kubwa ya watu wenye sifa walikuwa wanatoa taarifa za uongo wakati wa kukusanya taarifa za watu wenye sifa  za kunufaika na mpango wa TASAF,hatua ambayo imekuwa tatizo.
     Mwakilishi wa Mkurugenzi katika mkutano huo Steven  Vidoga anasemakuwa hakuna kijiji ambacho kimeachwa katika malipo bali serikali katika hatua za mwisho za kukamilisha taarifa za awamu ya mpango ilikuanza kutoa fedha na miradi kwa wanufaika.
     Vidoga amekanusha taarifa kwa wanufaika wa mpango  wa TASAF,zinazosemekana kusitisha  kwa mpango huo na kusema kuwa sio muda mrefu utaanza kutolewa kwa wanufaika.Pia kijiji cha Wnginyi kina wakazi zaidi ya elfu moja na kinaidadi kubwa  ya wazee na kaya zenye maisha duni lakini wanufaika 58 pekee ndio wanaopata fedha za TASAF.

No comments

Powered by Blogger.