Header Ads

Header ADS

Arch.Mwakalinga, ambana Mkandarasi anayejenga barabara ya Chunya-Makongorosi Mbeya.

     Arch.Elius Mwakalinga ambaye ni Katubu Mkuu wa Wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano(sekta ya ujenzi) amemtaka Mkandarasi anayejenga barabara ya Chunya-Makongorosi kwa kiwango cha lami kuhakikisha mradi huo unamalizika kulingana na makubaliano yaliyopangwa katika mkataba huo.
  Hata hivyo,amesema kulingana na muda aliopewa ulikuwa unamtosha kabisa kumaliza kazi kwahiyo hatomuongezea tena muda Mkandarasi huyo.
  Amezungumza hayo wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya wakati akikagua kiwango kilichofikia hadi sasa cha barabara hiyo imikiwemo na mambo mengine lakini hata hivo amemwambia Mkandarasi huyo kwamba ili kukamilisha ujenzi huo kwa muda muafaka anatakiwa aongeze vitendea kazi pamoja na wataalamu wengine.













   "Natarajia utaongeza vifaa na wataalamu ili kuhakikisha kazi hii inakamilika kwa wakati, pia ukumbuke kuwa sitakupa muda wa nyongeza hivyo fanya juhudi ili umalize mradi huu ndani ya muda", amesisitiza Arch. Mwakalinga.
Katibu Mkuu huyo amefafanua kuwa ujenzi wa barabara ya Chunya-Makongolosi yenye urefu wa KM 39 unajengwa na mkandarasi China Railway 15 Bureau Group Corporation kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 59 ambazo zote ni fedha za Serikali na unatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2020.
Aidha,Katibu Mkuu huyo amemtaka Mkandarasi huyo muda nwingi kuwa sehemu yake ya kazi lakini pia ikiwezekana kuongeza muda wa kufanya kazi hata usiku na mchana ili tu mradi huo kuweza kumalizika kwa wakati muafaka.
"Fanyeni kazi usiku na mchana ili kuepukana na changamoto za vipindi vya mvua na hakikisheni barabara hii inajengwa kwa viwango vya ubora zaidi", Arch. Mwakalinga amesema.
Lakini pia,Eng,Mwita Magesa ambaye ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Mwita Magesa, amemueleza Katibu Mkuu huyo kuwa mpaka sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 53 ukilinganisha na muda wa mkataba uliotumika ambao ni miezi 23 sawa na asilimia 85.19 ya muda wa mkataba.
Aidha,Eng.Mwita amesema kwamba hadi sasa Mkandarasi ameshafaniwa kujenga tabaka la juu la barabara kwa mawe yaliyosagwa KM 9.18, lami ya prime KM 6.78 na kazi zingine za ujenzi wa makalvati madogo na madaraja makubwa matatu yakiwa yanaendelea.
Barabara hiyo yenye urefu wa Km 39 ni sehemu ya barabara ya Mbeya-Rungwa ambayo inayounganisha Mkoa wa Mbeya pamoja na mikoa mingine ya jirani ya Singida na Tabora yenye urefu wa Km 293 ambapo fursa nyingi za kimaendeleo kwa wananchi,kiusafirishaji pamoja na kiuchumi mara tu baada ya kukamilika kwa barabara hiyo.
Imeandikwa na mwandishi >Adolf Mwingira.


No comments

Powered by Blogger.