Header Ads

Header ADS

Watuhumiwa 407 wa makosa ya uhujumu uchumi Nchini Tanzania wamekili na kuomba msamaha.

           Mkurugenzi wa mashitaka[ DPP ]Biswalo Maganga amewasilisha ripoti la watuhumiwa 407 waliokili na kuomba msamaha kwa makosa ya uhujumu uchumi.kwa rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli na kuongeza kuwa kiasi cha Shilingi bilioni 107 za Tanzania zitarejeshwa na watuhumiwa hao.
 Itakumbukwa kuwa Rais Magufuli alitoa wiki moja kuanzia Septemba 22 kwa watuhumiwa wote wa makosa ya uhujumu uchumi kukiri makosa yao, kuomba radhi na kurejesha kiasi cha fedha wanachoshitakiwa kuhujumu.
Magufuli
 Raisi Dr .Magufuli leo ameongeza tena wiki moja baada ya kuombwa na DPP Maganga ambaye ameeleza kuwa baadhi ya maombi yamekwama magerezani na kwenye ofisi zake za mikoa.Ikumbukwe kuwa Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, mashtaka ya uhujumu uchumi hayana dhamana, na wote wanaoshtakiwa nayo husalia rumande mpaka kutoka kwa hukumu zao.
"Najua wapo ambao wanadanganywa kuwa huu msamaha ni wa uongo, kuwa wakikubali watakuwa wamejishitaki wenyewe. Wengine wanadanganywa na mawakili ambao wanataka kuendelea kuwachomoa pesa zao. Sasa wachague kuwasikiliza mawakili au wewe DPP na ushauri wangu," amesema Raisi  Magufuli.
     Baadhi ya watu mashuhuri wanaokabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi ni mwanahabari wa uchunguzi Erick Kabendera.
    Erick .Kabendera anatuhumiwa kwa kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini Tanzania, shtaka la pili ni la kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja sabini za kitanzania.Pamoja na Wafanyabiashara maarufu Harbinder Sing Sethi na James Rugemalira wanaohusishwa na kashfa ya ufisadi ya Tegeta Escrow wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi.
Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Harry Kitilya, pamoja na maafisa wa benki ya Stanbic mlimbwende wa taifa wa zamani (Miss) wa Tanzania Shose Sinare na Sioi Sumari pia wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi.
Wengine waliopo mahabusu kwa mashtaka kama hayo ni viongozi wa kitaifa wa mpira wa miguu, bwana Jamal Malinzi na Michael Wambura ambao ni rais na makamu wa raisi wa zamani wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF).


    No comments

    Powered by Blogger.