Chadema wadai kuwa hawa wakurugenzi ni tatizo
Tumaini Makene ambaye ni mkuu wa idara ya habari na mawasiliano CHADEMA,ameeleza kuwa kutokana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ya Ubungo kushindwa kumuapisha Diwani wa viti maalumu,hali hiyo imepelekea kuhisi kuna mchezo mchafu unafanyika,lakini pia amekanusha kuhusu Madiwani wa halimashauri hiyo hawajagomea mkutano wa baraza.
Akizungumza na EATV,ambapo amemtaka Mkurugenzi wa Manispa hiyo kuhakikisha Diwani huyo anaondolewa vizuizi ili kuweza kumuapisha,kwani asipofanya hayo itakuwa anaenda kinyume na maadili pia maagizo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC,kwani ndiyo iliyomteua Anna Kajigiri kuwa Diwani wa viti maalumu.
''Walitarajia katika kikao hicho kwa mujibu wa ratiba Anna Kajigiri ataapishwa kuwa sehemu ya baraza,sasa Madiwani wenzake wanahisi kuna mchezo mchafu unafanyika kwenye ofisi ya Mkurugenzi,kutomuapisha tofauti na maelekezo ya NEC ambayo ilimteua Anna Kajigiri kuwa diwani halali wa halmashauri ya ubungo,kimsingi awajagomea mkutano isipokuwa wameeleza wasiwasi wao dhidi ya uzembe wa ofisi ya Mkurugenzi kushindwa kumthibitisha mwenzao kuwa diwani''.Makene amesema.
Kwa mujibu wa hali hiyo CHADEMA imemuomba Mkurugenzi huyo kumuapisha Diwani wao na kwamba yeye kama mtumishi wa umma si vyema kuweka mbele masuala ya kisiasa na kukiuka maagizo ya NEC,chombo ambacho kina mamlaka ya mwisho ya kumtangaza nani anafaa kuwa Diwani au Mbunge.

No comments
Post a Comment