Header Ads

Header ADS

Rais Magufuli afanya mkutana na Watendaji kata wa kata zote Nchini Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Dkt.John Pombe Magufuli Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amewaeleza watendaji kata wote nchi kutambua kuwa wao ndiyo wasimamizi wote wakuu wa kata zao kwahiyo wanaitajika kuwawajibisha wakuu wa mikoa na hata Mawaziri pale waendapo kinyume na maadili ya utawala bora katika kata zao.
  Hayo ameyasema leo Ikulu Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na watendaji wote kutoka Mikoa yote nchini mkutano huo,ambapo amesema kuwa watendaji wa ngazi za juu wakiukapo maadili bora ya utawala wanapaswa 'kumpa barua'na nakala zote kutumwa katika Ofis ya Rais.












  ''Kwenye yako kuna Mkurugenzi,Mkuu wa Mkoa au hata Waziri wewe Mtendaji kata ndiyo msimsmizi Mkuu.Hata kama kuna kiongozi wa nafasi gani yuko chini yako na anapoonekana anaenda visivyo unapaswa kumuwajibisha au hata kutoa taarifa kwa mamlaka yake''Magufuli amesema.
  ''Unaweza kumuandikia maoni,na usiogope hata kumlima barua hata kama anakuzidi cheo,eleza kwamba katika kata hii naona kiongozi huyu anaenda kinyume na maadili,alafu nakala unapiga hapa kwangu.Ni lazima tujifunze kuogopana.''Rais Magufuli ameongezea kusema haya.
    Hata hivyo Magufuli amewaitaji watendaji hao kuhakikisha wanachukua kero za wananchi na kuzitolea utatuzi pasipo kusubiri ziara ya viongozi wa ngazi za juu.
   Lakini pia ameeleza kuwa kiongozi anayekuwa karibu sana na wananchi ni Watendaji wa kata kwahiyo wanapaswa kutatua kero zao wananchi na pindi waonapo zipo juu ya uwezo wao wanatakiwa kuwasilisha kwa viongozi wa ngazi za juu.
    Aidha ameendelea kuwakumbusha kusimamia maagizo ya Serikali katika masuala mbalimbali kama vile ikiwemo na kufuta tozo za mazao chini ya tani moja na tozo nyingine zaidi ya 80 kwenye sekta kilimo na uvuvi.

No comments

Powered by Blogger.