Header Ads

Header ADS

Kassim Majaliwa atoa tamko katika mamlaka ya NIDA

    Kassim Majaliwa waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ametoa agizo katika mamlaka ya Usajili wa vitambulisho vya Taifa[NIDA] kusimamia na kuhakikisha wananchi wanapewa namba za utambulisho wa usajili wao kabla ya muda wa usajili wa laini za simu kuitimisha hususani kwa wananchi wanaoishi vijijini.













    Tamko hili ametoa wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha hospital ya wilaya ya Geita katika kijiji cha Nzela wakati akizungumza na wananchi.
  Aidha ameeleza kuwa hali ya  kuwapatia namba za utambulisho wa usajili wananchi ambao hawajapata vitambulisho vya uraia kitawezesha kuingia kwenye orodha ya wale wanosubiri kusajiliwa hata kama muda wa usajili utakuwa umeisha. Mwisho wa muda wa usajili ni Desemba mwaka huu.
  Hata hivyo,Waziri ameeleza kwamba Serikali imetoa vifaa vingi vya kisasa vya kielekroniki ili kuwezesha NIDA kufanya kazi zao kwa ufanisi na haraka lakini pia hali bado sio nzuri kwa sababu wanchini ni wengi ambao hawajapata vitambulisho hata hivyo kasi ya usajili wa laini za simu katika maeneo mengi kulalamikiwa.
  

    










   

“NIDA mnalalamikiwa, nimeenda Morogoro Vijijini NIDA mnalalamikiwa hivi utendaji wenu uko je? Kwanini mnachelewa ?” Waziri Mkuu alimuuliza Afisa Msajili wa NIDA wa wilaya ya Geita, Paschal Saro ambaye alijitetea kwamba wamesajili laini za simu 340 na tayari namba za usajili 330 zimeshatolewa.
   Saro alimwambia Waziri Mkuu kuwa suala la utata wa uraia kwa baadhi ya wananachi wanaoomba vitambulisho vya NIDA ni moja ya sababu zinazochelewesha usajili wa vitambulisho vya uraia.

Waziri Mkuu aliwasihi wananchi wote kuwa walinzi wa nchi yao kwa kutoa taarifa za watu ambao wanaomba viutambulisho vya uraia wa Tanzania wakati si raia na aliwataka watoe taarifa mara moja kwenye vyombo vya dola pale wanapogundua kuwa kuna raia wa nje anafanya mchakato wa kuapata vitambulisho hivyo.
    Aidha,Waziri mkuu amesema kuwa wamekamata baadhi ya silaha ambazo wananchi hawaruhusiwe kumiliki na zinasadikiwa kuingizwa nchini na raia wa nje wasiowaaminifu na Serikali kukamata silaha hizo katika mikoa ya mipakani ambayo ina wakimbizi.
  Lakini pa,Awali,Waziri Mkuu, alikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Geita iliyopo katika kijiji cha Nzera mkoani Geita na kufurahishwa na hatua ya Mbunge wa jimbo wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma ambaye amewezesha upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya hospitali hiyo.
     Kwa mujibu wa Waziri Mkuu ametoa pongeze kwa Msukuma kwa kuwa na moyo wa upendo dhidi ya wapiga kura wake.kwani vifaa hivyo vinastahili kuwa katika hospitali za rufaa za Mikoa kwa sababu ni vya kisasa,hata hivyo  mbunge huyo ameamua kuwapelekea wapiga kura wake kwenye hospitali ya wilaya dhumuni kuu ni kuweka uduma iliyokuwa bora na imara zaidi.

No comments

Powered by Blogger.