Header Ads

Header ADS

Magufuli apiga marufuku uchangishaji fedha machinjio ya Vingunguti

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameuagiza uongozi wa Hamashauri ya Ilala kutochangisha fedha katika machinjio ya Vingunguti hadi pale watakapokamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa.

     Amesema hayo, alipofanya ziara ya kushtukiza na kuwataka viongozi wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na watendaji wengine kuangalia namna ya kukamilisha kazi hiyo ili kuwaondolea adha wafanyabiashara wa maeneo hayo.
”Kuanzia sasa mkurugenzi wa Halmashauri na watendaji wengine ni marufuku kukusanya mapato ya aina yoyote” amesema Rais Magufuli. Pia amewataka viongozi hao kufanyia kazi maagizo yake usiku na mchana.
 Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa eneo hilo la machinjioni ambalo linadaiwa kukusanya takribani milioni 100 kwa mwezi.
Hayo yamezungumzwa  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza akitokea kwenye uzinduzi wa Rada na kiwanda cha mabomba ya plastiki kilichopo maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.