Header Ads

Header ADS

Uganda na Rwanda za fikia makubaliano ya kudumisha usalama

  Katika mkutano uliofanyika mjini Kigali uliowahusisha wajumbe wa Serikali ya Uganda na Rwanda,wameweka makubaliano kadhaa ikiwemo na kujiepusha na shughuliza kuyumbisha usalama katika nchi mojawapo.
    Kutokana na kukamilika kwa kikao hicho taarifa mojawapo ni kwamba,Rwanda imeeleza Raia wake wanaozurika nchini Uganda,na Serikali ya Uganda kukili kufanya uchunguzi wa kina taarifa hizo na kuhakikisha kwa wale watakaopatikana pasipokuwepo na hatia kuachiliwa huru.











Pande hizo zimekubaliana pia kusahihisha mkataba wa kuwarudisha makwao watuhumiwa wa uhalifu. Wajumbe kwenye mkutano huo wa mjini Kigali wamekubaliana na kuachana na tabia ya kutumia vyombo vya habari au mitandao ya kijamii, kwa kufanya propaganda ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa nchi zao.
     Hata hivyo,wamekubaliana pia kuhusu suala la usafirishaji wa vitu mipakani pamoja na watu katika nchi zao,katika kikao kitakachofuata kitakachofanyika Mjini Kampala suala hilo litajadiliwa,baada ya siku 30 zijazo.
      Ujumbe wa Uganda kwenye mkutano huo wa Kigali ulikuwa unaongozwa na waziri wa mambo ya nje, Sam Kutesa, nao ujumbe wa serikali ya Rwanda ulikuwa unaongozwa na waziri wa mashauri ya kigeni Olivier Nduhungirehe.
   Angola Manuel Domingos Augusto,ambaye ni Waziri wa mambo ya nje na Naibu Waziri Mkuu wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC,pia akiwemo na Gilbert Kankonde Malamba,ambaye ni Waziri wa mambo ya ndani na Usalama,waliudhuria katika mkutano huo kama wawakilishi wa wasuluhushi ambao ni marais wa Angola na DRC.
       Katika mwezi uliopita walipokutana mjini Luanda,Angola,Marais Yoweri Museveni wa Uganda pamoja na Paul Kagame wa Rwanda walikubaliana kupitia mazungumzo kumaliza mzozo wa kisiasa kupitia baina ya nchi zao.

No comments

Powered by Blogger.