Mashambulizi ya anga yavilenga vikosi vya vinavyoungwa mkono na Irani
Shirika la haki za kibinadamu la Syrian Observatory for Human Rights, lililo na makao yake nchini Uingereza limesema kwamba takriban wapiganaji 18 wa Iran na wale wanaoungwa mkono na Iran waliuawa.
Haijulikani ni nani aliyetekeleza mashambulio hayo usiku kucha ndani na nje ya mji wa Albu kamal.
Haijulikani ni nani aliyetekeleza mashambulio hayo usiku kucha ndani na nje ya mji wa Albu kamal.
- 'Salamu za amani ziwafikie Waafrika Kusini'
- Kasisi aliyelazimishwa kuwatengenezea mabomu Islamic State
- Trump: Mazungungo ya siri na Taliban ''yamekufa''
Lakini Israel imetekeleza mamia ya mashambulizi dhidi ya kambi za Iran nchini Syria wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Lengo la Israel ni kuangamiza kile inachokitaja kuwa uwezo wa kijeshi wa Iran nchini Syria mbali na usafirishaji wa silaha za Iran kwa makundi ya kijeshi kama vile Hezbollah nchini Lebanon.
Shirika hilo la haki za kibinadamu lilinukuu vyanzo vyake vikisema kwamba ndege hizo zisizojulikana zililipua kambi na hifadhi za zana na magari yanayomilikiwa na wapiganaji wa Iran katika eneo la al- Hizam al-Akhdar pamoja na maeneo mengine karibu na Albu Kamal.
Omar Abu Layla , mwanaharakati mwenye makao yake Ulaya kutoka kundi la DeirEzzor 24 , alisema kwamba milipuko mikubwa ilisikika katika mji huo na kwamba kulikuwa na ghasia na hofu miongoni mwa wapiganaji hao.
Kundi jingine kwa jina Sound and Pictures , lilinukuu maafisa wa afya waliosema kwamba takriban watu 21 waliuawa na kwamba wapiganaji walichukua mifuko yote ya damu katika hospitali ya Albu kamal ili kuwapona wapiganaji wao waliojeruhiwa'
Duru kutoka jeshi linaloungwa mkono na Iran zimesema kwamba ndege moja isio na rubani ililenga makao yake makuu katika mpaka wa Syria na Iraq takriban kilomita 6 kusini mwa Albu kamal.
Jeshi hilo lilituma magari kutoka mji uliopo karibu wa al-Qaim hadi katika eneo hilo ambalo lilikuwa na idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa duru hiyo iliongezea.
Jeshi la Israel halikutoa tamko lolote kuhusu kisa hicho , lakini liliripoti kwamba idadi kubwa ya mabomu ya roketi yalirushwa kuelekea Israel saa chache baadaye kutoka maeneo ya viungani vya mji mkuu wa Damascus.
Ilisema kuwa roketi hizo zilifeli kupiga maeneo ya Israel na kuwalaumu wapiganaji wanotekeleza operesheni zao chini ya jeshi la Iran Revolutionary Guard lakini ikasema kwamba inalaumu serikali ya Syria.
Wakati huohuo, Hezbollah imesema kwamba wapiganaji wake waliangusha ndege isiokuwa na rubani ya Israel katika anga ya kusini mwa Lebanon mapema siku ya Jumatatu na kuikamata.
Jeshi la Israel lilisema ndege yake moja ilianguka kusini mwa Lebanon wakati wa operesheni zake za kawaida, lakini haikutoa sababu , lakini ilisema kwamba hakuna hofu kwamba ujumbe iliokuwa ikikusanya utachukuliwa.
No comments
Post a Comment