Header Ads

Header ADS

Mitaala ya Elimu nchini Tanzania yapangwa kuboresha.

   Nchini Tanzania Serikali imesema imepanga kuboresha mitaala ya Elimu kama vile miundombinu ya elimu ya juu,kati,sekondari pamoja na shule za misingi lakini pia katika mitaala iliyopo iwapo inafaa kwa kipindi hiki cha sasa.
   Katibu mkuu wa wizara ta elimu,sayansi na teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo amebainisha hayo hapo jana wakati akifungua mkutano wa mwaka wa tathmini ya Elimu jijini Dododma.













  Aidha,ameeleza kuwa jitiana kubwa imekuwa ikifanywa na Wizara ya Elimu ili kuhakikisha kiwango cha elimu kinapiga hatua na kutoa elimu iliyo bora nchini,kwa kuanza na maboresho ya miundombinu ya elimu ya vyuo vya juu,elimu ya kati,shule za sekondari pamoja na shule za msingi.
   “Tumekuwa tukiboresha hali ya elimu yetu, na kwa sasa tumeanza na maboresho ya miondombinu ili vitu hivi viende kwa pamoja, madarasa kwa vyuo vya Kati na shule zetu zote ikiwepo Mzumbe na UDSM” amesema Dkt. Akwilapo.
Kuhusu maboresho ya Mitaala, Dkt. Akwilapo amesema utaenda sambamba na ile ya shule za msingi na vyuo, kwa kuzingatia matwaka ya usasa, kwa wanafunzi kuweza kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.                               
Aidha,Dkt.Akwilapo ameelezwa kwamba kwa sasa kiwango cha elimu nchini kimeimarika tofauti na awali na kwamba wengi wa wanafunzi wanaomaliza masomo ya sekondari hufanya vizuri katika mashindano ya taaluma nje ya nchini.                                                                          
“Wapo watu bado wana dhana ya kwamba elimu yetu haina viwango, jambo hilo si kweli kwani wanafunzi wanaomaliza masomo yao hapa nchini wakienda nje hufanya vizuri na kuiletea sifa nzuri nchi yetu.” Ameongeza Dkt. Akwilapo.                                                                                   
            Mwanzo wakati akizungumza kwenye mkutano huo,  Mwenyekiti wa mtandao wa Asasi za kiraia wadau wa elimu (TENMET), ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hakielimu John Kalage, amesema wanaridhishwa na hali ya elimu nchini.                                                                                    
“Na kupitia mkutano hu tutaangalia na kushiriki kujadili changamoto zilizopo katika elimu hasa ongezeko la udahili katika shule ili kusitokee athari za utoaji wa elimu isiyo bora kwa watoto wetu.” amefafanua Kalage.          
                                                

                                                                                            

No comments

Powered by Blogger.