Header Ads

Header ADS

Tanzania yafanya maojiano na mwakilishi wa WHO kuhusu taarifa za uchunguzi wa Ebola

       DKt.Hassan Abass ambaye nimsemaji mkuu wa Serikali ya Tanzania ameeleza katika ukurasa wa Twitter kuwa Dkt. Damas Ndumbaro, Naibu waziri wa mambo ya nje wa Tanzania ndiye aliye kutana na mwakilishi mkazi wa WHO Nchini Tanzania Dkt.Tigest Katsela Mangestu. 











    Kwa mujibu wa Dkt Abbasi serikali imemwita Dkt Mangestu ili kupata undani wa hoja za shirika hilo ambazo zimeripotiwa na vyombo vya habari.
         
Serikali imemwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa nchini kupata kwa kina hoja za Shirika hilo zinazosambaa kupitia vyombo vya habari. Mwakilishi huyo amesisitiza kuwa WHO haijasema wala haina ushahidi wowote kuwa TZ kuna Ebola na itashirikiana na Serikali.
 
        Aidha katika mazungumzo hayo Dkt.Abass amesema kuwa  "WHO imeafiki kuwa kama kuna mahitaji ya kupata taarifa zaidi kutoka Serikali ya Tanzania lazima utaratibu ulioanishwa katika miongozo ya taasisi hiyo na ambayo imeridhiwa na Serikali ifuatwe kikamilifu."
  Kwa upande wao WHO  imeeleza kwamba kufuatia taarifa zisizokuwa rasmi kuhusu visa vya ugonjwa na jitihada zake kupata taarifa kutoka kwa idara husika Tanzania kuhusu hali nchini humo, mpaka sasa hawajapokea data za kliniki, matokeo ya uchunguzi, mawasiliano na watu husika na hata matokeo ya uchunguzi wa maabara waliofanyiwa wagonjwa hao wanaoshukiwa.

No comments

Powered by Blogger.