Header Ads

Header ADS

Mkazi wa Nsongwi jijini Mbeya amuua mwanae kwa kumnywesha sumu.

   Silvia Sande [28] mkazi wa Nsongwi jijini Mbeya ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumuua mwanae mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili kwa kumnywesha sumu kali ya kuulia wadudu kisha nae mwanamke huyo kunywa sumu.
      Kwa maelezo ya Ulrich Matei,ambaye ni Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,amesema mnamo sa 4 asubuhi Septemba 16,2019 tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Nsongwi kilichopo kata ya Ijombe,Tarafa ya Tembela kata ya Mbeya vijijini.











     Aidha,Matei amesema kuwa mtuhumiwa alikunywa sumu ya kuulia wadudu chumbani kwake akiwa na dhumuni la kujiua na hata hivyo kumnywesha mwanae sumu hiyo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili anayejulikana kwa jina la Asifiwe Baini.
    Lakini pia baada ya tukio hilo mama huyo pamoja na mwanae walipelekwa katika kituo cha afya cha Igawilo na kwa bahati mbaya mtoto huyo alifariki.
    Kwa mujibu wa Kamanda Matei alisema mara baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani lakini kwa sasa bado Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia kwa mahojiano zaidi.

No comments

Powered by Blogger.