Header Ads

Header ADS

Kassim Majaliwa awataka Mawaziri wa SADC kusimamia Maendeleo ya Teknolojia.

    Kassim Majaliwa ambaye ni Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amewasisitiza Mawaziri wanaosimamia Tehama,habari pamoja na uchukuzi wa hali ya hewa kutoka nchi 16,wanachama wa jumuiya ya kusimamia maendeleo ya nchi kusini mwa Afrika SADC kusimamia maendeleo ya teknolojia.
     Wakati akizindua mkutano wa mawaziri hao hapo jana septemba 19,2019 amesema hayo,ambapo ulianza na majidiano yaliyowakutanisha Makatibu wakuu pamoja na viongozi wa juu wanaohusika na sekta hiyo kutoka nchi wanachama ambao walikaa siku tatu kabla ya baraza la mawaziri lililoanza juzi.
    Maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu ni pamoja na kushughulikia masuala ya Mtandao,mkakati wa posta kuurudisha katika Teknolojia ya sasa., kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya nchi na nchi, maendeleo kiteknolojia. Katika hotuba yake, amesema mkutano huo ni wa kwanza kisekta baada ya mkutano wa awali. 
      “Ni matarajio yetu kuwa mkutano huu utajadili utekelezaji wa mikakati mbalimbali, programu na miradi kama ilivyoainishwa kwenye mpango mkakati elekezi wa maendeleo ya sadc wa mwaka 2015 mpaka 2030. “Pamoja na mpango kabambe wa maendeleo ya miundombinu wa mwaka 2019 mpaka 2023 utajadili na kufanya tathmini na kuja na njia mbadala ya utekelezaji uchumi kikanda ili kuharakishwa,” alisema.













Nae Isack Kamwele ambaye ni waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchi wanachama pamoja na wakuu wa Taasisi na Mashirika pamoja na Viongozi waliopo katika Sekta binafsi nchi za SADC.
    Aidha katika majadiliano hayo amesema wote kwa pamoja wanazo changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika hali ya hewa,miundombinu mbalimbali ambayo inasababisha nchi kutijikwamua kiuchumi na pia wana mpango wa  pamoja katika kuzileta nchi kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wote.
.“Kipindi cha asubuhi tumeshaanza na tumeendelea na mjadala wajumbe walileta hoja mbalimbali kushuhghulikia reli, majanga na hali ya hewa, manufaa ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuboresha uchumi na maisha ya wana SADC. 














“Aidha wataalamu kutoka sekta za kibenki maendeleo ya Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini wameelezea uwezo wao katika kusaidia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu katika sadc, lakini pia maeneo mengine yaliyoangaziwa ni pamoja na ushirikishwaji wa wanawake na sekta binafsi,” amesema Kamwelwe.

No comments

Powered by Blogger.