Header Ads

Header ADS

Mpina awataka wafugaji kuongeza uzalishaji wa maziwa Nchini

Waziri wa Mifugo na  Uvuvi Luhaga Mpina amewataka wafugaji kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini ili kuchochea uwekezaji katika Tasnia ya Maziwa.
          Ameyesema hayo leo jijini Dare sSalaam katika mkutano na Waandishi wa habari  kuelekea siku ya unywaji wa maziwa shuleni Duniani itakayoadhimishwa Septemba 25 mwaka huu katika  mkoa wa Iringa.

   Pia amesema kuwa ni mikakati ya Serikali  kuhakikisha kuwa uzalishaji wa maziwa unaongezeka kutoka lita bilioni 2.7 hadi kufika lita bilioni 7 kwa mwaka ifikapo 2020 na kusema kuwa malengo ya Serikali  ifikapo mwaka 2025 kila shule ya msingi iwe na  programu za kunywa maziwa shuleni na kila mtanzania awe anakunywa angalau  lita 100 kwa mwaka.
       Mpina amesema kuwa  Kwa sasa kuna shule 25 tu ambazo zinatekeleza Programu ya unywaji maziwa shuleni na  kunufaisha jumla ya wanafunzi16.849 kwenye wilaya za Njombe, Mbeya na Wangingo'mbe. Kwa mjibu wa taarifa program hizi zinaendeshwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ,Viwanda vya kuzindika maziwa ,Wazazi pamoja na Wafadhili mbalimbali.Waziri Mpina ametoa pia rai kwa wananchi kunywa maziwa na bidhaa za maziwa ili kuchochea maendeleo ya Tasnia ya Maziwa.

Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa shuleni yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa uwanja wa Samora. Kauli Mbiu ya Maadhimisho haya ni Glasi moja ya maziwa kila siku kwa afya na  Elimu bora.


No comments

Powered by Blogger.