Header Ads

Header ADS

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Stephen Kebwe atumbuliwa.

  Lowata Sanare ateuliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro baada ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Stephen Kebwe kutumbuliwa.
     Hapo jana septemba 20,2019 ndipo Rais alitangaza uteuzi na utenguzi huo,Mhandisi John Kijazi ambaye ni katibu mkuu kiongzi balozi ameeleza kwamba Rais amefanya utenguzi na mabadiliko kadhaa.











  Lakini pia,Rais amemteua aliyekuwa msaidizi wa mkuu wa mkoa wa Geita Mussa Masele,kuwa mkuu wa Wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro.
    Pia ikumbukwe kwamba Rais Magufuli,Waziri mkuu pamoja na Dkt.Bashiru walishawai kumuonya Kebwe juu ya uendaji wake wa kazi.
     Aidha,katika ziara ya Waziri mkuu mkoani Morogoro Kebwe aliambiwa achunge mkoa wake kwani hali ni mbaya kila kona, ''Mkuu wa mkoa chunga mkoa wako hali ni mbaya,kila wilaya hali ni mbaya upotevu wa fedha mkubwa mno,mkoa wa Morogoro ni shida''
   Julai 25,wakati aliposimama kwa muda eneo la Kisaki mkoani morogoro na kuweza kuongea na wananchi wakati akielekea kufanya uzinduzi wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme katika bonde la Stigler katika Mto Rufiji alitoa onyo kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro.
     Aidha,Rais Magufuli alimweleza kuwa siku nyingine akipita Morogoro na kukuta tatizo hilo la mifugo ya wafugaji kupeleka katika mashamba ya wakulima linaendelea ataona viongozi hawatoshi.
  Aidha Dk Kebwe jana alipozungumza na gazeti la Mwananchi kuelezea utendaji kazi wake na maoni yake juu ya matamko ya viongozi hao wa juu na hali tete ya wadhifa wake alisema kuwa hatua zimekuwa zikichukuliwa na kitendo cha Waziri Mkuu ni cha kupigilia msumari kile wanachokifanya.
    Kufuatia uteuzi huo Rais amefanya mabadiliko kadhaa ambayo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amehamishiwa wilaya ya Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime.

No comments

Powered by Blogger.