Header Ads

Header ADS

Wakili Fatma Karume asimamishwa kazi.

Kufuatia kesi iliyofunguliwa na Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo,Ado Shaibu akipinga Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).Mahakama kuu ya Tanazania imeamua kumsimamisha Wakili Fatma Karume asiendelee kuwa Wakili kwa muda.

   









Wakili huyo amedai maamuzi hayo yamefanywa bila yeye kusikilizwa.Serikali kwa upande umelalamikia matamshi yaliyotolewa na Wakili huyo katika kesi iliyofunguliwa dhidi ya Rais John Pombe Magufuli na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
    Ado Shaibu ametoa taarifa hiyo kupitia Ukurasa wake wa Twiter ambapo amesema kuwa.
”Kesi yangu dhidi ya Rais Magufuli imeondolewa “struck out” kwa kumjumuisha Mh. “John Pombe Magufuli”. Wakili wangu Fatma Karume atafafanua.
Wakili Fatma Karume amesimamishwa (suspended) uwakili kwa maneno yake kwenye “submission” ya kutetea kesi yangu” amesema Ado Shaibu.
   Jaji kiongozi wa Tanzania Dkt Eliezer Feleshi ametoa uamuzi huo jana Septemba 20,2019 lakini pia ameiondoa kesi hiyo kwa kuwa imemjuisha na Rais Dkt John Magufuli.
Fatma Karume ni mwanasheria, wakili wa kujitegemea, mwanaharakati ambaye aliwahi kuwa rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019.

No comments

Powered by Blogger.