Header Ads

Header ADS

Mwandishi wa habari anashikiliwa Tanzania Erick Kabendera afanyiwa vipimo.

       Erick Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari za kiuchunguzi Nchini Tanzania anayetuhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi,ameiambia Mahakama nchini humo kuwa ameanza kupelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa vipimo.
    Wakati alipopandishwa kizimbani septemba 12,Kabendera alionekana kuuvuta mguu wake na kuonekana kwenye maumivu na mawakili wake kuieleza mahakama kuwa mteja wao ana matatizo ya kupumua kwa shida pia kupooza mguu wa kulia.

 









   Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi leo hii,Kabendera amethibitisha kwamba jana jumanne septemba 17,2019 amefanyiwa kipimo cha X Ray kwenye mgongo wake pamoja na kipimo cha damu katika hospitali ya Rufaa Amana.
    "Nashukuru jana nilifanikiwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Amana na nilifanyiwa kipimo cha X Ray kwenye mgongo wangu na majibu yametoka," amedai Kabendera.
    Aidha,kwa mujibu wa Kabendera ameeleza kwamba alichukuliwa kipimo cha damu hata hivyo majibu yake bado hajapewa na yanasubiliwa ili aanze matibabu.
   Pia ameieleza mahakama kuwa bado ana maumivu makali katika mguu wake.
      Lakini kwa upande wa mashtaka umeeleza kwamba bado haujakamilisha upelelezi na Augustine Rwizile ambaye ni hakimu wa mkazi mwandamizi wa mahakama ya Kisutu ameahirisha kesi hiyo hadi mnamo Oktoba 1,2019.

No comments

Powered by Blogger.