Header Ads

Header ADS

Mwenge wa Uhuru umegoma kufungua mradi wa ujenzi wa mamilioni Njombe.

Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2019 zimeshindwa kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji kijiji cha Kidegembye jimbo la Lupembe wilayani Njombe mkoani Njombe.Akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua na kupitia nyaraka za ujenzi wa mradi huo amesema mwenge wa uhuru umeshindwa kuweka jiwe la msingi katika mradi huo kutokana na kubaini ukiukwaji wa utaratibu wa ujenzi.
      











                                                                                                                    “Lakini maji yapo safi na salama ndugu wananchi muweze kuyatumia hayana shida yoyote,ambayo yamejitokeza hapa ni kwa wataalamu kuto kuweza kusimamia vizuri kwasababu hizi ni fedha za wananchi lazima zisimamiwe kipengele hadi kipengele”alisema kiongozi wa mbio za mwenge.
          Wakati akisoma taarifa ya mradi huo Injinia wa maji halmashauri ya wilaya ya Njombe, Rajabu Yahaya kwa niaba ya mkurugenzi, amesema hali halisi ya utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 90% ya kukamilika ambapo mpaka sasa wananchi wanapata huduma ya maji huku mradi huo ukiwa umeanza kutekelezwa machi 7,2018 na mkandarasi MSSTC construction limited kwa gharama ya shilingi bilioni moja.
   Ikiwa ni miradi sita imekaguliwa na kufunguliwa na mbio za mwenge wa uhuru kitaifa wilayani Njombe mkoani Njombe huku kiongozi wa mbio za mwenge akitoa pongezi kwa halmashauri hiyo katika utekelezaji wa miradi.

     

No comments

Powered by Blogger.