Header Ads

Header ADS

Mwili wa aliyekuwa Raisi wa Zimbabwe Robart Mugabe wawasili Zimbabwe kutoka Singapore

          Mugabe, alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1980. Alikuwa madarakani kwa karibu miongo minne kabla ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi mwaka 2017.
Atazikwa siku ya Jumapili baada ya shughuli za maziko siku ya Jumamosi.
Mwili wa Mugabe umepelekwa kwenye makazi ya familia ''Blue Roof'' mjini Harare.
Mwili wa Mugabe ukiwasili
Siku ya Alhamisi na Ijumaa, Mwili wa Mugabe utalala katika uwanja wa mpira wa Rufaro eneo la Mbare mjini Harare, ambapo ndipo alipoapishwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Zimbabwe baada ya kupatiwa uhuru kutoka kwa koloni la kiingereza mwaka 1980.
Taratibu za kitaifa za kuuaga mwili wake zitafanyika siku ya Jumamosi ,kwenye uwanja wenye uwezo wa kupokea watu 60,000 kabla ya kuzikwa kijijini kwao Jumapili.
Rais wa taifa hilo Emmerson Mnangagwa ametaja kuwa ''shujaa wa taifa'' kwa jitihada zake za kuisaidia Zimbabwe kupata uhuru wake.
Lakini ripoti zinasema kuwa Mugabe hakutaka waliomuondoa madarakani kushiriki katika maziko yake, hivyo badala yake huenda shughuli za maziko zikafanywa kwenye makazi ya familia yake.
         Familia ya Mugabe inapinga mpango wa serikali wa kumzika katika makaburi ya mashujaa wa taifa katika mji mkuu wa Zimbabwe -Harare na wanataka azikwe katika kijiji alikozaliwa.
Wengi miongoni mwa mashujaa wa taifa la Zimbabwe - wale ambao walishirikiana katika mapambano dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache wamezikwa katika eneo la makaburi ya Mashujaa lililopo nje kidogo tu ya mji mkuu Harare.
Mugabe ambaye anakumbukwa na wengi kama mkombozi ambaye aliwaondoa watu wake katika pingu za ukoloni wa wazungu walio wachache anakumbukwa na wengine kama mtu aliyeangusha uchumi wa moja ya chumi zilizotazamiwa kufanya vizuri zaid barani Afrika na ambaye aliwatesa kikatili wapinzani wake.   

No comments

Powered by Blogger.