Header Ads

Header ADS

Ngorongoro Heroes yashuka dimbani jumapili dhidi ya mechi na Unganda.

      Ngorongoro Heroes ambayo ni timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 20,imefanya safari yake kutoka Mjini Jinja kuelekea Mjini Gulu,ambapo pana umbali zaidi ya kilomita 400 kwa ajili ya kupiga mchezo wa robo fainali utakaopigwa hapo juma pili dhidi ya Uganda.
   Ambapo katika michuano ya CECAFA U20 Chalinje Cup inayondelea nchini hapa Tanzania Bara ilimaliza ikiwa ni vinara wa kundi B,hivyo inakutana na Uganda ambayo ilishika nafasi ya 3 katika kundi A hapo kesho.











  Kheeled Muhamed ambaye ndiye mkuu wa msafara huo amezungumza kwamba hali ya wachezaji wote ipo vizuri isipokuwa mchezaji mmoja tu ambaye ni golikipa Ally Salim ambaye mchezo uliopigwa dhidi ya Kenya alipata majeraha.
    “Timu imeondoka hapa Jinja leo asubuhi kwenda Gulu ikiwa kwenye hali nzuri kabisa. Lengo letu ni kufanya vizuri kuhakikisha tunakwenda mbele zaidi ikiwezekana kuondoka na kombe,” alisema Mohammed.
  Hata hivyo amesisitiza kwa kusema “Kwa kifupi mipango yote iko vizuri. Kama viongozi tunahakikisha wachezaji wetu wanapata kila wanachohitaji ili waweze kushindana,”.
   Ambapo Timu hiyo ya Tanzania Bara imeweza kuonyesha kiwango kikubwa katika michezo iliyopigwa ambapo iliweza kuibuka na ushindi dhidi ya Ethiopia ambapo ilishinda bao 4-0  lakini pia Zanzibar 5-0 huki ikiibuka na sare ya 2-2 dhidi ya Kenya.
     Lakini pia,michuano hiyo ya  robo fainali zitachezwa siku ya Jumapili na Jumatatu kwenye miji ya Jinja na Gulu. Mechi nyingine za robo fainali ni Eritrea na Zanzibar, Sudan Kusini na Sudan Kaskazini huku Kenya ikicheza na Burundi.

No comments

Powered by Blogger.